Maarifa hupunguza woga. – Enock Maregesi
Author : Enock Maregesi
Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua. – Enock Maregesi
Ukiwa na elimu huna sababu ya kuwa maskini. – Enock Maregesi
Ukiwa karibu na Mungu utakuwa na maarifa kuliko profesa, Mungu ana maarifa kuliko profesa. – Enock Maregesi
Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO. – Enock Maregesi
Tunapenda kuamini kwa sababu kuamini hurahisisha mambo… Usiamini. Jua. – Enock Maregesi
Elimu ni ufunguo wa maisha lakini wengine funguo zao zina kutu! – Enock Maregesi
Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu! – Enock Maregesi
Maarifa ni mbegu ya mabadiliko. – Enock Maregesi
There are many internal secrets that make a person continue to succeed, and there are many external secrets that make a person continue to hide their secrets. Internal secrets are true secrets, while the outer secrets are false secrets, aimed at hiding the truth. However, the secret to success is hard work, knowledge and secrecy. […]